Syria 'yaridhia' mpango wa amani

arab league Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Mzozo umedumu miezi saba

Shirikisho la nchi za Kiarabu limesema Syria imekubaliana na wito wake wa kumaliza makabiliano na wapinzani wa serikali yaliyodumu kwa miezi saba

Waziri mkuu wa Qatar ametangaza kuwa mazungumzo yao na Syria yamefaulu na ameongeza kuwa itakuwa kheri zaidi ikiwa waliokubaliana yataanza kutekelezwa mara moja.

Kuliangana na shirikisho la nchi za kiarabu, Syria itaondoa majeshi yake kutoka mitaani nchini humo, itawaachia huru wafungwa wa kisiasa na itaandaa mazungumzo ya kitaifa na viongozi wa upizani katika kipindi cha wiki mbili zijazo.

Katika mazungumzo hayo, serikali ya Syria pia imeridhia kuwa waandishi wa habari na waangalizi kutoka shiriksho hilo wataruhusiwa nchini humo kushuhudia matukio hayo.

Hata hivyo utawala wa Syria mjini Damascus haujadhibitisha makubaliano hayo.

Viongozi wa upinzani nchini humo pia wanashuku sana ikiwa Rais Bashar al- Assad atatekeleza ahadi hizo.

Ghasia zilikuwa bado zinaendelea nchini humo licha ya kuwa mazungumzo hayo yalikuwa yanaendelea.

Hata hivyo utwala wa Syaria umekuwa ukilaumu magaidi na magenge yaliojihami na silaha kuwa ndio yanatekeleza maafa mengi yanayotokea nchini humo.

Vyama vya upizani vinasema ikiwa kweli jeshi la Syria litaondoka kwenye barabara za mji mkuu, basi Rais Assad atakuwa hatarini ya kupoteza ushawishi wake nchini humo.