Syria yawaachilia wafungwa wengi

Syria inasema imewaachilia huru watu 553 ambao walikamatwa wakati wa maandamano nchini, kuadhimisha siku kuu ya Idd.

Haki miliki ya picha Reuters

Taarifa ya shirika la habari la taifa ilisema wale waliofunguliwa hawajamwaga damu.

Huku nyuma shirika linalotetea haki za kibinaadamu nchini Syria liliarifu kuwa watu watatu wameuliwa kwa bunduki za rashasha katika mji wa Homs Jumamosi, na wanamgambo wane wa serikali waliuwawa katika mapambano na wanajeshi walioasi, kaskazini mwa nchi.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, Nabil al-Arabi amesema ikiwa juhudi za jumuiya hiyo zitashindwa kutatua mzozo wa Syria, basi itakuwa maafa kwa kanda hiyo.

Serikali ya Syria ilikubali juma hili kuondoa wanajeshi wake mitaani na kuanza mazungumzo na upinzani.