Malema amaliza kujieleza

Kiongozi wa tawi la vijana la chama cha ANC, Afrika Kusini, Julius Malema -- anahudhuria kikao cha mwisho leo kutazama vitendo vyake.

Haki miliki ya picha Getty

Anaweza kutolewa katika chama cha ANC iwapo atakutikana na makosa ya kuvunja heshima ya chama na kuleta mgawanyiko chamani.

Kisa hicho kilianza pale Bwana Malema alipotoa wito kuwa serikali ibadilishwe katika nchi ya jirani ya Botswana.

Ameomba msamaha kwa matamshi hayo.

Julius Malema alikuwa akimuunga mkono Rais Zuma tangu alipochukua uongozi wa chama, lakini wanasiasa hao wawili sasa hawapatani.

Matokeo ya vikao hivyo vya chama yatatolewa baada ya siku kadha.