Tsvangirai avunja mkutano wa hadhara

Mkutano wa hadhara ulioitishwa na Waziri Mkuu wa Zimbabwe, Morgan Tsvangirai, umevunjwa, baada ya wafuasi wake kushambuliwa na vijana kwa mapanga, mitarimbo na mawe.

Haki miliki ya picha AFP

MDC inasema watu 20 walipelekwa hospitali; na inawalaumu wafuasi wa Rais Robert Mugabe katika mji wa Chitungwiza, kusini ya Harare.

Fujo dhidi ya MDC zimezidi katika majuma ya karibuni wakati matayarisho yanaanza kwa uchaguzi unaotarajiwa kufanywa mwaka ujao.