Dalai Lama ashutumu serikali ya China

Dalai Lama Haki miliki ya picha AFP
Image caption Dalai Lama

Kiongozi wa kidini kutoka jimbo linalotaka kujitenga la Tibet ambaye anaishi uhamishoni, Dalai Lama amelaumu China kwa kile amekitaja kuwa ukandamizaji dhidi ya raia wa Tibet.

Akizungumza mjini Tokyo, Dalai Lama amesema ukandamizaji unaoendelezwa na utawala wa China umepelekea raia wengi wa Tibet kuanza kujitia kitanzi hasa katika mkoa wa Sichua.

Takriban watu wanane wamejiua kwa kujiteketeza kupinga utawala wa China katika jimbo la Tibet.

China hata hivyo imemlaumu Dalai Lama ikisema ndiye aliyechochea vitendo hivyo.