Msimamo wa China muhimu kwa vikwazo

Kufuatia Ripoti ya shirika linalosimamia masuala ya nuclear IAEA kuhusu mpango wa Iran wa Nuclear mtazamo sasa umegeuka kutoka ya kiufundi na kuwa ya kisiasa ambapo Marekani pamoja na nchi za magharibi zinataka kuzidi kuishinikiza Iran kwa kuiwekea vikwazo zaidi.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Iran yakana kujenga silaha

Urusi tayari imeonyesha hasira juu ya Ripoti hio ikisisitiza tangu mwanzo kua utaratibu mwingine unaweza kuifanya serikali ya Iran isalimu amri.

Ripoti mpya ya shirika linalosimamia masuala ya Nuclear ndio chagizo kuu ambayo Marekani na Mataifa makuu ya magharibi yanataka kutumia kama sababu ya kuiwekea Iran vikwazo zaidi vya kiuchumi.

Marekani inatumai kwamba Mkutano wa IAEA baadaye mwezi huu utaweza kuipeleka ripoti yake mbele ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.

Lakini Urusi na Uchina huenda yasiunge mkono hata ikiwa ripoti hio itafikishwa mbele ya vBaraza la usalama na hilo linaweza likasabaisha vikwazo vipya visipitishwe.

Mataifa ya magharibi yanaweza kuachwa bila mbinu ila kukaza vikwazo vyao binafsi. Lakini bila Urusi na Uchina vikwazo vya aina yoyote havitokua na makali.

Nchi moja hasa, Uchina imeibuka kua chachu katika kuishinikiza Iran. Biashara baina ya Mataifa hayo inazidi kuimarika. Mnamo mwaka 2009 Iran ilikua nchi ya pili katika nchi zinazoiuzia Uchina mahitaji yake ya nishati.

Uchina kwa upande wake huiuzia Iran theluthi ya mahitaji yake ya petroli. Katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita biashara baina ya nchi hizi imepanda kwa asili mia 40.

Makampuni ya Uchina yana sehemu kubwa ya soko la simu za mkononi huko na mahusiano yamefikia kiwango cha kubadilishana bidhaa pale ambapo malipo ya fedha taslmu yamekwamishwa na vikwazo.

Juhudi za Marekani kuishinikiza Uchina isizidi kushirikiana na Iran mara kadhaa zimegonga mwamba.

Makampuni ya Uchina yana sehemu kubwa katika soko la simu za mkononi nchini Iran kwa mfano.

Urafiki baina ya mataifa haya umekua kiasi kwamba Iran na Uchina yamekua yakijadili kwa kina biashara ya kubadilishana bidhaa badala ya kutumia fedha taslimu kutokana na vikwazo dhidi ya Iran.

Kiu ya Uchina ya mafuta inalifanya Taifa hilo liwe na mtazamo tofauti na ule wa Marekani kuhusu Mataifa ya Ghuba.