Iran yapuuza ripoti ya UN

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais wa Iran akikagua mradi wa nuklia

Iran imekosoa vikali ripoti ya shirika la Umoja wa Mataifa la kawi ya atomiki IAEA, ambayo inadai kuna ishara inatengeneza zana za kinuklia.

Shirika hilo la IAEA halikuweka bayana maelezo kwamba nchi hiyo inaunda bomu la nuklia, lakini ripoti yake inaashiria kwamba utafiti wa kisayansi unaofanyika nchini Iran unaonyesha kuwa ina mipango ya kijeshi.

Iran imeshutumu matokeo hayo na kusema yamechochewa kisiasa.

Nchi hiyo imekuwa ikikanusha tuhuma kwamba inaunda zana za kinuklia na kusema kuwa inarutubisha madini ya uranium kwa uzalishaji wa kawi kwa matumizi ya uma wake.

Kwa matokeo ya ripoti hiyo Marekani sasa inapendekeza kuwa nchi hiyo iwekewe vikwazo zaidi.