Malema asubiri hukumu

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Malema: Kiongozi wa vuguvugu la vijana wa ANC anayekabiliwa na tuhuma za ukosefu wa nidhamu

Kamati ya nidhamu ya chama tawala cha African National Congress, ANC, nchini Afrika kusini itatoa hukumu dhidi ya kiongozi wa tawi la vijana wa chama hicho, mwenye utata na ushawishi mwingi Julius Malema .

Malema ambaye ameshtakiwa pamoja na maafisa wengine watano anashutumiwa kuchochea mgawanyiko na kuvunja heshima ya chama hicho.

Malema pia amekuwa akizozana na kiongozi wa chama hicho Rais Jacob Zuma.

Anaweza kutolewa katika chama cha ANC, iwapo atapatikana na makosa.

Kwa mjibu wa mwandishi wa BBC aliyeko kusini mwa Afrika kutimuliwa kwa Malema huenda kukadidimiza ushawishi wake kuhusu atakayekuwa kiongozi wa nchi hiyo mwakani