Mkataba wa bwawa la Congo

Afrika Kusini na Jamhuri ya Demokrasi ya Congo, zinatarajiwa kutia saini leo, za kufufua tena ule mpango wa kujenga bwawa kubwa kabisa duniani la kutoa umeme.

Haki miliki ya picha

Rais Jacob Zuma, wa Afrika Kusini anazuru Congo ili kutia saini mkataba huo.

Iwapo litajengwa, bwawa hilo la Grand Inga, linakisiwa kuwa litagharimu dola bilioni-80, na litazalisha umeme mara mbili zaidi ya bwawa la Uchina la Three Gorges.

Juhudi za zamani za serikali ya Congo na wawekezaji wa kiamataifa zilishindwa kufanikiwa kutumia nguvu za maji ya mto Congo.