Kampeni za uchaguzi zaanza Morocco

Kampeni zimeanza nchini Morocco za uchaguzi wa wabunge baada ya katiba mpya kuanza kutumika mapema mwaka huu, ambayo imempa waziri mkuu na bunge madaraka zaidi.

Haki miliki ya picha AFP

Uchaguzi utafanywa mapema kwa karibu mwaka mzima, kujaribu kutekeleza mabadiliko yaliyopendekezwa na Mfalme Mohammed haraka zaidi.

Lakini waandamanaji waliofanya mihadhara kwa miezi kadha kudai uwazi katika siasa, wametoa wito wa kususia uchaguzi huo.

Wamelaani mabadiliko hayo ya katiba kuwa ni pambo tu.