Sudan yatuhumiwa kuadhibu wanaharakati

Shirika la kutetea haki za kibinaadamu, Amnesty International, limeishutumu serikali ya Sudan kuwa inawaadhibu na kuwatendea vibaya wanaharakati kadha wa upinzani ambao wameshiriki katika maandamano ya karibuni.

Haki miliki ya picha Reuters

Amnesty inasema watu zaidi ya 100 walikamatwa mwezi wa Oktoba katika eneo la mji mkuu, Khartoum, baada ya kuandamana kupinga bei zinazopanda.

Wengi kati ya hao waliokamatwa wameadhibiwa, pamoja na kupigwa mateke na kuzuwiliwa kulala.

Wakuu wa Khartoum hawakusema kitu juu ya tuhuma hizo.