Wenye HIV wadai haki Malawi

Kikundi cha wanawake wa Malawi wanaofanya kazi ya ukahaba, kinaishtaki serikali baada ya kulazimishwa kukaguliwa kama wana HIV, bila ya kuombwa ruhusa.

Wanawake hao 14 wanasema haki yao ya kuweka mambo hayo siri, imekiukwa; siyo tu walipokaguliwa, lakini piya matokeo ya ukaguzi yalipotajwa hadharani mahakamani.

Wanawake hao walikuwa wameshtakiwa kwa kufanya ukahaba huku wakiwa na ugonjwa wa kuambukiza.

Kesi yao inaungwa mkono na mashirika ya Malawi ya kutetea haki za kibinaadamu.

Malawi ni kati ya nchi zenye kiwango kikubwa cha magonjwa hayo duniani.