Marekani yaomba msamaha

Marekani imeomba msamaha kwa rais wa zamani wa India, Abdul Kalam, baada ya kupekuliwa katika uwanja wa ndege wa New York mwezi wa September.

Haki miliki ya picha Getty

Serikali ya India ililalamika kuwa maafisa wa usalama, walimpekua Bwana Kalam, kabla na baada ya kupanda ndege; na kwa muda mfupi walilichukua koti na viatu vyake.

Katika barua ya kuomba msamaha, serikali ya Marekani ilisema kuwa taratibu zinazofaa za kupekua waheshimiwa hazikufuatwa katika tukio hilo.

Ombi la msamaha hilo linafuatia tukio kama hilo mwaka wa 2009, wakati mchezaji sinema wa India, Shah Rukh Khan, alidai kuwa alizuwiliwa kusailiwa katika uwanja wa ndege Marekani, kwa sababu ya jina lake la Kiislamu.