Zao la Muhogo katika hatari ya kuangamia

Muhogo Haki miliki ya picha other
Image caption Muhogo

Wanasayansi wa Umoja wa Mataifa wanaonya kuwa virusi vinavyoushambulia mmea wa Muhogo vimeenea katika sehemu kubwa ya Afrika.

Muhogo ni moja ya mazao muhimu zaidi duniani ambayo huwapa watu wengi theluthi moja ya lishe ya kila siku.

Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa linasema hali hii inahitaji kushughulikiwa kwa haraka na limeomba kuongezwa kwa fedha za kulishugulikia suala hilo.

Aina ya mbegu za muhogo zilizogawanyiwa wakulima katika bara la Afrika zinaonesha kukabiliana na virusi hivyo.

Muhogo ni chakula muhimu duniani ambacho barani Afrika ni muhimu zaidi kwa kuwa muhogo unawezqa kukuazwa katika udongo ambao ambao huna rotuba na eneo ambalo halina mvua ya kutosha.

Lakini kama mazao mengine muhogo hukabiliwa na tatizo la wadudu na virusi ambavyo hukwamisha uzalishaji wake. Usambaaji wa Virusi mara kwa mara umefanikiwa kutokomeza kabisa zao hilo katika baadhi ya maeneo na kusababisha njaa.

Sasa shirika hilo la FAO linasema kuna virusi vingine vipya ambavyo vimeanza kutishia zao hilo katika Afrika Mashariki.

Wanasayansi wanasema virusi hivyo ambavyo husababisha ugonjwa unaojulikana kama "Cassava Brown Streak Disease" ama CBSD vinaelekea kusambaa mbali zaidi nakuleta hasara kubwa katika zao hilo.Virusi hivyo vilionekana kwa mara ya kwanza nchini Uganda mwaka 2006 lakini miezi michache iliyopita vimeone Burundi na katika Jamhuri ya kidemocrasia ya Congo kwa mara ya kwanza.