Sudan Kusini italipia mapatano

Sudan Kusini inasema iko tayari kumlipa jirani yake, Sudan Kaskazini, mabilioni ya dola ili kumaliza mizozo ya hivi sasa, pamoja na eneo la mzozo la Abyei.

Haki miliki ya picha AFP

Mpatanishi mkuu wa Sudan Kusini, Pagum Amum, alisema wamekabidhi mapendekezo hayo kwa serikali ya Khartoum, kumaliza mizozo kuhusu Abyei, mafuta, mizozo ya mipaka na usalama.

Alisema nchi yake inataka kuepuka vita kwa njia yoyote ile.

Pamezuka mapigano karibuni katika majimbo kadha kaskazini kidogo ya mpaka baina ya nchi mbili hizo.