Wanajeshi wa Ethiopia wako Somalia

Msemaji wa Rais Sharif Sheikh Ahmed wa Somalia, ameiambia BBC kwamba hana habari kwamba wanajeshi wa Ethiopia wako ndani ya nchi yake.

Haki miliki ya picha AP

Msemaji huyo, Suldan Farah alisema wanajeshi wa Ethiopia wako sehemu za mpakani, wakiwafunza wanajeshi wa serikali ya Somalia na kuwapa msaada wa usafiri.

Msemaji huyo alisema uhusiano baina ya Somalia na Ethiopia ni mzuri, na nchi mbili hizo zinatayarisha mpango wa kuwashinda wapiganaji wa Kiislamu wa al-Shabaab.

Waliowaona wanajeshi wa Ethiopia wanasema wako katika mji wa Guri'el, katikati mwa nchi, na kwamba wanazungumza na wanamgambo wanaounga mkono serikali, wa Ahlu Sunna, na ambao wanadhibiti eneo hilo.