Saif azuwiliwa pahala siri

Maafisa wa mashtaka wa Libya wataanza kumhoji Saif Al-Islam Gaddafi leo Jumapili katika pahala siri, ambako anazuwiliwa baada ya kukamatwa hapo jana.

Haki miliki ya picha Reuters

Afisa wa wizara ya sheria ameiambia BBC, kwamba Bwana Luis Moreno Ocampo, mkuu wa mashtaka wa Mahakama ya Jinai ya Kimataifa, ICC, anatarajiwa kukutana na Saif atapozuru Libya juma lijalo.

Saif al-Islam anatakiwa na ICC kwa mashtaka ya uhalifu wa vitani.

Serikali ya mpito ya Libya, imeiahidi ICC kwamba Seif atafanyiwa kesi ya haki nchini Libya.