Tazama ramani na michoro ya DRC

Imebadilishwa: 25 Novemba, 2011 - Saa 12:49 GMT

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ni nchi yenye sifa tele. Ni kubwa mno na yenye utajiri mkubwa wa madini kama vile almasi na dhahabu, hata hivyo hali ya maisha ni duni sana miongoni mwa raia wa nchi hiyo

Tumia ramani na michoro hii kuona nchi hii kubwa iliyopo kwenye bara la Afrika, nchi iliyopitia maumivu makubwa , huku ikijiandaa kwa uchaguzi wake wa pili tu kufanyika katika kipindi cha miongo minne.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
UKUBWA
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ina ukubwa wa kilomita za mraba 2,344,858 katikati mwa Afrika, na kuifanya nchi hiyo kuwa ya 12 kwa ukubwa duniani
UTAJIRI WA MADINI
Kongo ina utajiri mkubwa wa madini.Ina zaidi ya 70% ya madini ya Koltani duniani, inayotumika kutengenezea sehemu muhimu ya simu za mkononi, Ina 30% ya hifadhi ya almasi duniani na kiwango kikubwa cha kobalti, shaba na boksiti. Hata hivyo utajiri huu umewavutia waporaji na kuchochea vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.
USAFIRI
Licha ya ukubwa wa nchi hiyo, miundo mbinu ni duni.Miongoni mwa barabara zenye kilomita 153,497, kilomita 2,794 pekee ndizo zenye njia ya waenda kwa miguu. Kuna takriban kilomita 4,000 za reli lakini upana kati ya reli ni ndogo na ziko katika hali dhaifu.Mikondo ya maji ni muhimu katika kusafirisha bidhaa ndani ya nchi lakini safari hizo huenda taratibu na mara nyingine huchukua miezi tele.
WATU
Kukiwa na takriban watu milioni 71, DR Congo ni nchi ya nne yenye watu wengi zaidi Afrika.Takriban 35% ya watu huishi mijini na mji mkuu wa Kinshasa ndio mkubwa, ukiwa na zaidi ya wakazi milioni 8. DR Congo ina takriban makabila 200 wengi wakiwa kabila la Kongo, Luba na Mongo.
DATA
Kwa kuzingatia ukubwa na raslimali DR Congo inatakiwa kuwa nchi yenye mafanikio, lakini miaka mingi ya kugubikwa na vita, ufisadi na kutosimamia uchumi uzuri umeiacha nchi hiyo katika umaskini mkubwa. Kwa mujibu wa utafiti wa mwaka 2011 nchi hiyo imebaki nyuma sana katika maendeleo, huku wastani wa mategemeo ya umri wa kuishi ukiongezeka kwa miaka miwili tu tangu mwaka 1980, baada ya muda ambao kwa hakika ulishuka katika miaka kati ya 90.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.