Bahrain kufanya mageuzi ya kisiasa

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mfalme wa Bahrain Hamad Isa Bin Khalifa kufanya mageuzi ya kisiasa

Mfalme Hamad Isa Bin Khalifa wa Bahrain ameahidi kufanya mageuzi ili kuepuka ukiukwaji wa haki za binaadamu.

Hatua hiyo imekuja baada ya repoti ya Tume huru kuishutumu serikali kwa kutumia nguvu kupita kiasi katika kuzima maandamano. ".

Mfalme Hamad alielezea masikitiko yake kuhusu matokeo ya ripoti hiyo na kuapa kuhakikisha kwamba "matukio hayo machungu hayarudiwi tena".

Ripoti hiyo iliyokuwa inasubiriwa kwa muda mrefu kuhusu matukio ya February na March ilisema idadi kubwa ya waandamanaji waliozuiliwa waliteswa.

Zaidi ya watu 40 walikufa katika ghasia hizo ambazo baadhi ya maafisa waliilaumu Iran kwa kuchochea.

Wakazi wengi wa Bahrain ni wa madhehebu ya kiislamu ya Kishia na vitendo hivyo vya utumiaji nguvu vimechochea hasira dhidi ya ukoo wa Kifalme na tabaka la wanasiasa ambao ni wa madhehebu ya Sunni. .

Zaidi ya watu 1,600 walikamatwa wakati wa maandamano ambayo yaliendelea kila mahali tangu kufikia kilele kwa ghasia hizo miezi minane iliyopita.

Mkuu wa tume hiyo, Profesa Cherif Bassiouni, alisema wachunguzi wake hawajapata ushahidi wazi kwamba Iran ilihusika katika matukio ya Bahrain.

Prof Cherif aliwahi kuwa mwanasheria wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya haki za binaadamu na wajumbe wengine wa tume hiyo wote ni raia wa kigeni.