Wafungwa kwa upenzi wa jinsia moja

Image caption Paul Biya, Rais wa Cameroon

Wanaume watatu nchini Cameroon wamehukumiwa miaka mitano jela kwa kufanya mapenzi ya jinsia ambavyo ni ni kinyume na sheria za taifa hilo lililo Afrika ya kati.

Watuhumiwa wawili walikuwa mahakamani katika mji mkuu Yaounde, lakini mtu wa watu alihukumiwa akiwa hayupo.

Polisi walisema watu hao walikamatwa kwa kukutwa wakifanya mapenzi kwenye gari.

"Inatisha na ni uamuzi usiokubalika," Mwanasheria wa Cameroon na mwnaharakati wa haki za wapenzi wa jinsia moja Alice Nkom aliliambia shirika la habari za AFP.

"Si sawa kwa nchi inayozungumza juu ya haki za binadamu," alisema.

Mwandishi wa BBC Randy Joe Sa'ah aliyeko Yaounde anasema hofu imesambaa nchini Cameroon, kama katika baadhi ya nchi nyingine Afrika.

Anasema pamoja na miaka mitano jela, adhabu kubwa ya kufanya mapenzi ya jinsia moja nchini Cameroon – wanaume hao walitakiwa kulipa faini ya Francs 200,000 CFA francs (sawa na $400, £260).

Wakili wao Michel Togue alisema ni hukumu mbaya na anamtuhumu jaji kwa kuchanganya kesi hiyo na uchochezi, shirika la AFP liliripoti.

Wanaume hao wawili walikataliwa dhamana mwezi Agosti. Mshtakiwa wa tatu alipewa dhamana baada ya kukamatwa mwezi Julai na hakutokea mahakamani wakati kesi yake inasikilizwa.

Bi Nkom, anayeongoza shirika la kiraia la kutetea wapenzi wa jinsia moja ameaimbia BBC kuwa Agosti hakukuwa na ushahidi dhidi ya watu hao na walikamatwa kwa sababu walionekana kama wanawake na nywele zao ‘walitengeneza kama wanawake’

"Hili ni kosa la kimitindo, sio wapenzi wa jinsia moja," alisema.

Shirika la kutetea haki za Binadamu limesema sheria ya kuzuia mapenzi ya jinsia moja ni kali, ya kibaguzi na haina budi kufutwa.