Vikwazo dhidi ya Syria vyakubaliwa

Mawaziri wa Jumuia ya nchi za Kiarabu wamepiga kura kuiwekea Syria vikwazo, ili kuifanya serikali ya nchi hiyo iache kukandamiza maandamano kwa nguvu.

Haki miliki ya picha Reuters

Kati ya vikwazo hivyo ni kuzuwia wakuu wa Syria kuzuru nchi za Kiarabu, kusimamisha maingiliano na benki kuu ya Syria, na kuacha kuweka rasilmali nchini humo.

Waziri wa Mashauri ya Nchi za Nje wa Qatar,, Hamad bin Jassim, alisema uamuzi huo unafaa kutekelezwa mara moja.

Lakini alisema majirani wa Syria wanaofanya biashara kubwa nayo, yaani Iraq na Libnan, hazikuunga mkono azimio hilo, na zinasema hazilitekeleza.