Wamekusanyika tena Tahrir

Maelfu ya watu wamekusanyika tena Medani Tahrir mjini Cairo, mkesha wa uchaguzi wa bunge - uchaguzi wa kwanza tangu Rais Mubarak kuondolewa madarakani.

Haki miliki ya picha AFP

Waandamanaji wanajaribu kuendelea na shime ya chagizo kutaka serikali ya kijeshi ikabidhi madaraka kwa raia.

Mkuu wa serikali hiyo Field Marshall Hussein Tantawi, amesema uchaguzi wa bunge utafanywa kesho kama ulivopangwa, ingawa kuna ghasia za kisiasa.

Alisema kuwa hataruhusu kundi lolote lile kulichagiza jeshi.

Baadhi ya makundi ya upinzani yanataka uchaguzi uahirishwe.

Lakini chama cha Muslim Brotherhood hakitaki uchaguzi kucheleweshwa.

Kinatarajiwa kupata idadi kubwa ya viti vya bunge.