Uchaguzi wa wabunge Misri

Maandamano medani Tahrir Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Maandamano medani Tahrir

Wapiga kura katika miji mikubwa nchini Misri wanajiandaa kwenda kwenye vituo vya kupigia kura kuwachagua wabunge wao muda mfupi ujao.

Huu ni uchaguzi wa kwanza kufanyika nchini humo tangu kung'olewa madarakani kwa Rais Hosni Mubarak mwezi Februari, mwaka huu.

Mkuu wa baraza hilo, Field Marshall Hussein Tantawi, amewataka raia wa Misri kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi wa wabunge.

maandamano yaendelea

Baadhi ya vikundi vya upinzani vinataka uchaguzi huo uahirishwe, lakini kikundi cha Muslim Brotherhood, ambacho kimeimarika kisiasa kuliko vyote, kinataka uchaguzi huo ufanyike bila kucheleweshwa, huku maelfu ya waandamanaji wakiendelea kuwepo Medani Tahrir.

Waandamanaji wanataka baraza la kijeshi ambalo linashikilia madaraka, likabidhi madaraka hayo kwa serikali ya kiraia.

mlipuko

Wakati huo huo, habari kutoka Misri, zinasema watu wanaoshukiwa kuhujumu uchumi wa nchi hiyo, wamelipua bomba la kusambazia gesi asilia katika nchi za Israel na Jordan katika jangwa la Sinai, ikiwa ni saa chache kabla ya kuanza kwa uchaguzi wa wabunge.

Mlipuko umetokea karibu na mji wa Arish, Kaskazini mwa jangwa la Sinai, Misri.

Ni mara ya tisa kwa bomba hilo la gesi kushambuliwa mwaka huu, ikiwa ni baada ya kuong'olewa madarakani kwa Rais Hosni Mubarak.

Misri inaiuzia Israel karibu nusu ya gesi yake katika mkataba unaokosolewa vikali, ambao ulifikiwa wakati wa rais aliyeondolewa.