Kimberly Process imeshindwa Zimbabwe?

Haki miliki ya picha online
Image caption Almasi Zimbabwe

Shirika la Global Witness limesema linajiondoa kwenye Kimberly Process, mpango wa kimataifa ulioundwa kusimamisha biashara inayodaiwa kuwa ni za almasi haramu zinazotumika kugharamia vita.

Mpango huo uliundwa mwaka 2003, licha ya kuwa na wasiwasi kuwa mauzo ya almasi hizo zilikuwa zikitumika kufadhili vurugu kwenye nchi za Afrika kama vile Angola na Sierra Leone.

Ulihitaji almasi ghafi zote ambazo zitauzwa kimataifa zithibitishwe.

Lakini Global Witness limesema Kimberly Process imeshindwa kuvunja uhusiano uliopo baina ya mauzo ya almasi na vurugu.

Katika miaka ya 90, shirika hilo liliongoza kampeni ili kutoa uwazi wa tatizo hilo la ghasia kutokana na almasi hizo, pamoja na mashirika mengine yasiyo ya kiserikali ilikuwa ni muhimu katika kuunda mpango huo wa Kimberly Process.

Hata hivyo, kwa sasa, mpango huo umekosa imani na mfumo huo.

Muasisi wa Global Witness Charmian Gooch ameiambia BBC, "Takriban miaka tisa baada ya Kimberly Process kuanzishwa, ukweli unaosikitisha ni kwamba wanunuzi wengi hawawezi kuwa na uhakika ni wapi almasi zao zinatoka."

Alisema, "Mpango huo umeshindwa mitihani mitatu."

"Ilishindwa kupambana na biashara iliyoleta vurugu kutokana na almasi huko Ivory Coast, haikuwa radhi kuchukua hatua madhubuti katika kukabiliana na ukiukaji wa sheria uliofanywa na Venezuela katika miaka kadhaa na imedhihirisha kutokuwa na nia ya kuzuia almasi kuchochea ufisadi na vurugu Zimbabwe."

Makundi ya kueteta haki za binadamu yamekuwa yakionyesha wasiwasi kuhusu mfumo huo kwa muda sasa.

Mwezi Novemba, Kimberly Process ilikubali rasmi kuruhusu makampuni mawili kuuza almasi nje ya nchi kutoka eneo la Marange yanapochimbwa madini hayo nchini Zimbabwe.

Uamuzi huo ulitolewa licha ya madai kutoka Human Rights Watch na Global Witness kuwa jeshi la Zimbabwe limehusishwa na udhalilishaji wa haki za binadamu kwenye maeneo ya machimbo.