Ajali ya Bhopal yakumbukwa

Polisi wa India wamepambana na maelfu ya waandamanaji, waliojaribu kuzinga reli huko Bhopal, siku ya kukumbuka maafa makubwa kabisa duniani yaliyosababishwa na sumu kuvuja kutoka kiwanda, ambayo iliuwa watu kama 15,000 mwaka wa 1984.

Haki miliki ya picha PTI

Maelfu zaidi walijeruhiwa, na wengi bado wanaishi na athari zake.

Waandamanaji wanataka fidia zaidi kutoka kampuni ya Dow Chemicals, ambayo ilinunua kampuni iliyokuwa na kinu cha gesi hapo Bhopal, Union Carbide.

Wanaharakati piya wanataka kampuni ya Dow isiruhusiwe kuwa mfadhili wa michezo ya Olimpiki ya 2012 yatayofanywa London.

Dow inasema makubaliano ya awali yalimaliza madai ya fidia.