Ivory Coast yakaribia uchaguzi

Jumuia ya nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS, inasema kuwa itatuma ujumbe wa wachunguzi 60 kusimamia uchaguzi wa bunge nchini Ivory Coast tarehe 11 Disemba, kufwatia ombi la serikali.

Haki miliki ya picha AFP

Huo ni uchaguzi wa mwanzo kufanywa tangu uchaguzi wa rais wa mwaka jana uliokuwa na utata, na ambao ulizusha vita vilivouwa watu 3,000.

ECOWAS imesema uchaguzi wa bunge ni hatua muhimu katika ujenzi mpya wa taifa, maendeleo, na kukuza demokrasi nchini Ivory Coast.