Khartoum yateka kambi ya SPLA

Jeshi la Sudan linasema kuwa limeiteka kambi muhimu ya wapiganaji katika mkoa wa Kordofan Kusini.

Haki miliki ya picha AP

Eneo hilo liko kwenye mpaka baina ya Sudan Kusini na Kaskazini, na jeshi linasema kambi hiyo ilikuwa ya wapiganaji wa SPLA-Kaskazini, ambao walipigania Sudan Kusini katika vita virefu vya huko.

Haiwezekani kuthibitisha taarifa hiyo ya jeshi kwa sababu Sudan imepiga marufuku waandishi wa habari na mashirika ya misaada katika eneo hilo.

Serikali za Kahrtoum na Juba zinalaumiana kuwa zinasaidia makundi ya wapiganaji katika maeneo ya mpaka wao