Taharuki ya kisiasa yatanda DRC

Kiongozi wa upinzani Etiene Tshikendi Haki miliki ya picha

Kanisa Katoliki katika Jamhuri ya Kidemokasia ya Congo limetoa wito wa utulivu kudumishwa wakati taifa likisubiri matokeo ya mwisho ya uchaguzi a bunge na wa urais.

Askofu Mkuu (Nicholas Djombo) alitoa wito kwa maafisa wa uchaguzi kuhakikisha kuwa matokeo yaliyochapishwa kutoka uchaguzi wa Jumatatu iliyopita yako sahihi.

Alionya kuwa mizozo inaweza kusababisha machafuko makubwa.

Matokeo yaliyopatikana hadi sasa, ambayo juu kidogo ya nusu ya vituo vyote vya upigaji kura, yanampatia Rais aliye madarakani, Joseph Kabila aslimia arobaini na tano ya kura.

Mpinzani wake mkuu, Etienne Tshisekedi, ambaye amepata aslimia thelathini na nne ya kura, amepinga matokeo hayo ya awali , akisisitiza kuwa kura zimeibiwa.

Matokeo ya mwisho yanatarajiwa kupatikana siku ya Jumanne.

Taharuki imetanda mjini Kinshasa huku raia wa kigeni wakilazimika kuhamia taifa jirano la Jamuhuri ya Congo{Brazzaville}. Aidha huduma za mawasiliano ya simu za mkononi zimebanwa na serikali imesema baadhi ya wahalifu wanatumia ujumbe wa simu ya mkononi kuwatisha raia.