Gavana wa zamani Marekani afungwa jela

Gavana wa zamani Illinois Haki miliki ya picha Getty

Mahakama moja nchini Marekani imemhukumu gavana wa zamani wa jimbo la Illinois, Rod Blagojevich kifungo cha miaka kumi na minne jela kwa makosa ya rushwa, ikiwemo kujaribu kuuza kiti cha u-seneta kilichoachwa wazi na Rais Barack Obama.

Jaji wa mahakama hayo James Zagel amesema madhara ya vitendo vya gavana huyo havipimwi katika thamani ya fedha au mali, bali katika mmomonyoko wa maadili ambapo umma unapoteza imani kwa serikali.

Akiwa amekamatwa miaka mitatu iliyopita, Mr Blagojevich awali alikanushakutenda uovu huo, lakini wakati kesi ikiendelea kusikilizwa alisema yeye ndiye anayestahili kulaumiwa katika kashfa hiyo.

Hata hivyo jaji alisema kuomba msamaha kwa gavana huyo kumechelewa sana.

Waendesha mashtaka wamesema Bwana Blagojevich alitumia vibaya madaraka ya ofisi yake tangu awe gavana mwaka 2002.