Makubaliano mapya EU bila Uingereza

Wanachama wa Muungano wa Ulaya wanaotumia sarafu ya Euro wamekubali mpango mpya wa kodi na bajeti kutatua mzozo wa madeni.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais Sarkozy wa Ufaransa na Angela Merkel wa Ujerumani katika mkutano wa mzozo wa madeni ukanda wa Euro

Lakini jaribio la Ujerumani na Ufaransa kushawishi nchi wanachama 27 wa Muungano wa Ulaya kuunga mkono mabadiliko ya mikataba wa Ulaya liliashindikana baada ya pingamizi kutoka Uingereza.

Waziri mkuu wa David Cameron alisisitiza Uingereza isihusishwe katika baadhi ta mabadiliko kadhaa ya kifedha.

Badala yake wanachama wa ukanda wa Euro na wengine wamefikia makubaliano kwa kauli moja pamoja na adhabu kuwepo kwa kuvunja masharti yanayodhibiti nakisi.

Sheria mpya na ngumu kuhusu matumizi na bajeti sasa zitazitasaidiwa si na mkataba wa Muungano wa Ulaya lakini na mkataba kati ya serikali.

Itakuwa rahisi kuweka mipango lakini ambayo haiko moja kwa moja, Mhariri wa Ulaya wa BBC Gavin Hewitt anasema akiwa Brussels.

Lakini anasema Ulaya imechukua hatua kubwa kuelekea kwenye muungano huku kukiwa na sheria zinazowafunga zaidi kuhusu kodi na matumizi na vikwazo dhidi ya nchi zenye matumizi makubwa.

Mzozo wa madeni ya kitaifa Ulaya haujapata suluhisho.

Mkutano wa viongozi wa Ulaya mjini Brussels umeelezwa kuwa wa kufa na kupona kwa nchi 17 wanachama wa ukanda Euro.

Ufaransa na Ujerumani zikishinikiza mkataba mpya ubuniwe kuweka kanuni mpya za kifedha za kuzuia sarafu ya Euro isilipuke na Ulaya isisambaratike.

Mazungumzo ya karibu saa 10 hayakuweza kuzaa matunda matunda ya mapatano yanayoungwa mkono na wanachama wote wa Muungano wa Ulaya.

Uingereza na Hungary hazitoshiriki katika mapatano mapya ya kiserikali, ilhali Sweden na Jamhuri ya Uczec kwanza zitajadili hayo katika mabunge yao, kabla ya kufanya uamuzi.

Ingawa, wanachama 17 wa ukanda wa Euro, watashughulikia maafikiano tofauti nje ya mikataba ya Umoja wa Ulaya, Huenda wakaungwa mkono na takriban nchi nyengine nane.

Hatua muhimu zilizoafikiwa zinazoitwa ‘mkataba wa hazina’ ni kwamba:

  • nakisi ya bajeti ya nchi iwe na tama ya 0.5% ya zao ghafi la ndani au (gdp) kwa mwaka;
  • ‘matokeo ya madhara’ kwa nchi ambazo nakisi za serikali huzidi 3% ya zao ghafi la ndani;
  • maafikiano hayo mpya yaingizwe katika katiba za nchi wanachama;
  • Mfumo wa Utulivu wa Ulaya kuanza kutumika katika Julai 2012;
  • utoshelevu wa kikomo cha euro 500bn (au $666bn) kwa Mfumo wa Utulivu wa Ulaya;
  • nchi za ukanda wa Euro na nyIngine za Ulaya ziweke Euro bilioni 200 katika shirika la Fedha-IMF,
  • kutumiwa kwa msaada wa wanachama wa ukanda wa Euro wenye shida ya madeni.

Chancellor wa Ujerumani Angela Merkel, ameusifu mpango huo na kusema utachangia kuiokoa sarafu ya euro.