Muafaka wa mazingira unakaribia

Mazungumzo ya Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa yanayofanywa Afrika Kusini, yanaendelea kwa siku moja zaidi.

Haki miliki ya picha Reuters

Wajumbe wanaelekea polepole kukaribia muafaka kwamba utaratibu wa kutafuta makubaliano mepya ya kupunguza gesi inayoharibu mazingira, uanze mwaka mpya. Mswada unaosambazwa hivi sasa unasema kwamba viwango vilivowekwa sasa havitoshi kuzuwia joto duniani lisizidi nyuzi mbili za Celsius.

Richard Muyungi, ambaye anaongoza ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo unaofanywa Durban, alisema nchi zinahitaji kusimama kidete hadi zifikie makubaliano:

"Si lazima kufanya miujiza, lakini binaadamu tunaweza kung'angania lengo.

Mabadiliko ya hali ya hewa yanatuathiri sote, na tuko hapa kwa lengo moja.

Ni swala muhimu lenye utata.

Nina matumaini kuwa kila mmoja wetu anajitahidi tupate mafanikio.

Na natumai tukikutana mwishowe, tutaweza kukubaliana."