Wapalestina wakerwa na Gingrich

Wakuu wa Palestina wamemlaumu vikali mgombea urais wa chama cha Republican cha Marekani, Newt Gingrich, kwa kuwaelezea Wapalestina kuwa ni kabila lilovumbuliwa, ambalo linataka kuiangamiza Israil.

Haki miliki ya picha Reuters

Waziri Mkuu wa Palestina, Salam Fayyad, alisema matamshi ya Bwana Gingrich ni duni na ya kuaibisha; huku afisa mwengine wa Palestina, Saeb Erekat, alisema ni ya kudharauliwa.

Bwana Erekat alisema matamshi kama hayo yanaendeleza tu ghasia.

Bwana Gingrich hivi sasa anaonekana kuwa anaongoza katika mashindano ya kuwa mgombea urais wa chama cha Republican.