Upatanishi waanza Libya

Rais wa Serikali ya Mpito ya Libya amesema uongozi mpya uko tayari kusamehe vikosi vilivopigana kwa niaba ya Muammar Gaddafi.

Haki miliki ya picha jupiter still

Mustafa Abdel Jalil alitangaza kuwa Libya mpya itamjumuisha kila mtu.

Alisema hayo alipofungua mkutano wa upatanishi mjini Tripoli.

Wajumbe kutoka makabila makuu ya Libya wanahudhuria mkutano huo.