Waliouawa Syria 'wafikia watu 5,000'

Haki miliki ya picha UNIS
Image caption Pillay asema watu zaidi ya 5000 wauwawa Syria

Zaidi ya watu 5,000 wanaaminika kuuawa katika maandamano ya nchini Syria, afisa wa ngazi za juu wa haki za binaadamu wa Umoja wa Mataifa amesema.

amewaambia wajumbe wa Baraza la Usalama kuwa watu 14,000 wanaaminika kukamatwa na wengine 12,400 wamekimbia hadi katika nchi jirani.

Takriban watu 20 waliuawa katika makabiliano ya siku ya Jumatatu, wanaharakati wa upinzani wanasema.

Licha ya fujo, uchaguzi ulifanyika, lakini idadi ya watu waliojitokeza kupiga kura inasemekana kuwa ndogo.

Serikali inasema kuwa uchaguzi umekuwa huru zaidi kuliko miaka iliopita, lakini upinzani ulitoa wito wa kususia uchaguzi na kuanzisha mgomo.

Shirika la habari la serikali nchini Syria linasema watu wengi wamejitokeza katika vituo vya kupiga kura.

Lakini katika ngome za upinzani wanaharakati wanasema hakuna dalili kama uchaguzi unafanyika, na hata pengine hakuna hata mmoja anayepiga kura, mwandishi wa BBC Jonathan Head aliye nchi jirani ya Uturuki anasema.

Navi Pillay anaelezea hali nchini Syria kama "isiyoweza kuvumiliwa" na kusema kuwa mateso dhidi ya binaadamu huenda yalifanyika.

Bi Pillay anasema makadirio yake ya mauaji ya watu zaidi ya 5,000 hayajumuishi maafisa wa usalama. Serikali ya Syria inasema kuwa zaidi ya maafisa 1,000 wa polisi na jeshi wameuawa.