Bendera ya Iraq yapanda Baghdad

Bendera ya Marekani yafungashwa
Image caption Bendera ya jeshi la Marekani yashushwa

Sherehe yenyewe ilikua wakati wa kuvutia huku bendera ya Marekani ikiondolewa na badala yake ikiwekwa ile ya Iraq. Bendera hiyo ya Marekani ilifungiwa kwenye kifuriushi na daima hatotumika tena ikimaanisha kua ndiyo mwisho wa operesheni ya wa Marekani nchini Iraq.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Bendera ya Iraq ilipandishwa badala ya ile ya Marekani

Lililobaki ni biashara ya kiufundi ya kuwaondoa askari elfu chache waliosalia huko, waliopungua kutoka zaidi ya kambi mbili badala ya zaidi ya kambi mia 500 wakati operesheni ilipopamba moto.

Mpango huu wa kuondoa vikosi unatarajiwa kufikia tamati katika siku chache zijazo, ikiwa lengo ni mwisho wa kipindi chao cha mwisho wa mwezi huu,

Kwenye sherehe ya kuhitimisha operesheni hio karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad, Waziri wa Ulinzi wa Marekani Panetta na wwengine waliwasifi Aqskari wa Marekani na wengine waliopoteza maisha yao katika kipindi cha miaka kumi iliyopita na kusema walijitoa maisha yao ili Iraq iwe nchi yenye uhuru na usalama na pia Taifa lenye hadhi ya kujivunia.

Bw.Panetta alisema kua Marekani itaendelea na sera yake ya kuhifadhi jeshi lake katika eneo zima na pia kujenga uhusiano mwema na Iraq kupitia Ubalozi wake mjinibAGHDAD, ambao ni mkubwa kuliko balozi zote za Marekani duniani.

Hata hivyo mtazamo wa raia wengi wa Iraq ni kwamba ushawishi wa Marekani huko Iraqw unapungua, ukiifanya hata Iran kuweza kuimarisha mipango na ushawiushi wake kutoka nje ya mipaka baina ya nchi hizo mbili.

Katika ishara ya kuwepo mabadiliko ya kisiasa, ingawa viti vingi viliwekwa alama za waalikwa kutoka jeshi la Iraq, ni maaofisa wachache kutoka jeshi la Iraq waliohudhuria sherehe hio.