Morocco yapiga marufuku Uvuvi wa EU

Haki miliki ya picha na
Image caption Morocco yapiga marufuku uvuvi wa kigeni kwenye bahari yake kuu

Morocco imeamuru meli zote za kigeni zinazovua samaki katika eneo lake la bahari kuu chini ya mkataba wa Muungano wa Ulaya kuondoka haraka.

Hatua hiyo imekuja baada ya bunge la Ulaya kupiga kura kutoongeza mkataba wake ambao Muungano wa Ulaya uliilipa Morocco kuhifadhi samaki wake.

MEPs inasema mkaba huo haukuwa halali kwa kuwa haukuwapa faida watu wanaoishi katika eneo lenye mgogoro la Sahara Magharibi, ambalo uvuvi mkubwa uanfanyika.

Wizara imeema uamuzi wa bunge ni wa’kusikitisha’

Katika taarifa, imesema kuwa hatua hiyo ingekuwa na ‘athari zaidi kwa uhusiano kati ya Morocco na Muungano wa Ulaya kwenye uvuvi.

Muungano wa Ulaya na Morocco ni wabia wakubwa wa biashara umekuwa ukiilipa Euro 36milioni (£30milioni; $47milioni) Morocco kwa mwaka kwa kibali cha kuvua samaki katika bahari yake kuu, kimsingi katika pwani yake ya Sahara Magharibi.

Rasmi mkataba huo uliisha mwezi Februari na Muungano wa Ulaya ulitaka kuingia mkataba mpya mpaka mwezi Februari mwakani.

Lakini Jumatano, MEPs wakitumia nguvu zao walitoa amri chini ya mkataba wa Lisbon wakapiga kura kati ya 326 kura 296 zilikubali kuzuia mkataba mpya wakisema hakukuwa na ushahidi wa kutosha kuonyesha kuwa mkataba huo unawafaidia wananchi wa Sahrawi ambao ndio wanaishi Sahara Magharibi.

Wakosoaji wa wa mkataba huo wansema ilikuwa ni kupoteza fedha za umma na ulisababisha kuvua kupita kiwango.

Morocco iliivamia Sahara Magharibi mwaka 1976 lakini madai yake kuwa ni eneo la utawala wake hayajatambuliwa na jumuiya ya kimataifa.

Vuguvugu la kutenganisha Polisario lilipigana vita vya msituni dhidi ya vikosi vya Morocco mpaka mwaka 1991 na bado inatafuta kutambuliwa kama taifa huru.

Bunge la Ulaya limesema mkataba mpya hauna budi kujadiliwa ambalo linachukua suala la Sahara Magharibi katika umuhimu wake.