Gabon yachagua bunge

Uchaguzi wa bunge unafanywa nchini Gabon, Afrika Magharibi; nchi ambayo imeongozwa na ukoo wa Bongo tangu mwaka wa 1967.

Haki miliki ya picha bbc

Rais Ali Bongo alirithi madaraka baada ya baba yake, Omar Bongo, kufariki miaka mitatu iliyopita; na chama chake kinatarajiwa kushinda leo kwa urahisi.

Chama kikuu cha upinzani kinasusia uchaguzi huo.

Gabon ni nchi ya nne ya Africa inayotoa mafuta kwa wingi, na ina watu milioni moja na nusu tu.

Hata hivo zaidi ya nusu ya watu wa Gabon wanaishi kwenye umaskini.