Bunge la Iraq lagawanyika

Pande kubwa kabisa la wabunge wa Iraq limetoka kwenye ukumbi wa bunge, ili kulalamika juu ya mamlaka mengi aliyonayo Waziri Mkuu, Nouri al-Maliki katika uamuzi wa serikali.

Haki miliki ya picha AFP

Kundi hilo liitwalo Iraqiya, ambalo halielemei kwenye dini, na la waziri mkuu wa zamani, Iyad Allawi, limeitia nchi katika msukosuko wa kisiasa, siku chache baada ya wanajeshi wa Marekani kuondoka.

Kundi hilo lenye robo ya viti 325 vya bunge, limetaka kufanywe mazungumzo na serikali inayoongozwa na Washia, ili kutatua swala hilo.

Iraqiya ilishinda karibu kura zote za Wasunni wa Iraq, ambao ni wachache.