Polisi wa Kenya auawa kwa mlipuko Daadab

Haki miliki ya picha online
Image caption Eneo linalomilikiwa na al-Shabab Somalia

Mlipuko karibu na kambi kubwa zaidi ya wakimbizi duniani nchini Kenya umemuua afisa polisi mmoja, polisi wamesema.

Maafisa wawili walijeruhuwa wakati kitu kinachosadikiwa kuwa ni bomu kutupwa karibu na kambi ya wakimbizi ya Daasda, shirika la habari la Reuters linaripoti.

Kambi hiyo yenye kuhifadhi wakimbizi wapatao 450,000 ambao wamekimbia njaa na mapigano nchini Somalia.

Afisa mmoja wa Kenya aliambia BBC kuwa anahisi ni wapiganaji wa Kisomali walihusika na mlipuko huo.

Kenya imetuma vikosi vyake nchini Somalia kuwafuatilia wapiganaji wa kiisalm wa Al-Shabab kutokana na matukio ya utekaji nyara.

Al-Shabab linasema uvamizi wa Kenya ni kitendo cha kivita na italipa kisasi.

"Tulisikia mlipuko na tulipofika tuliona gari limechanwa vipande viwili. Kipande cha mbele kilikuwa juu ya mwili wa dereva ulioharibika," Naibu Mkuu wa polisi Dadaab Nelson Kaliti aliliambia Reuters.

"Polisi wengine wawili walipotolewa kwenye mabaki ya gari hilo wkiwa wamejeruhiwa vibaya," alisema.

Kaimu mkuu wa wilaya ya Daadad Bernard Ole Kipury amekiambia kipindi cha BBC cha Focus on Africa kuwa wanashuku al-Shabab wanahusika na mlipuko huio.

"Ni njia ya al-Shabab kulipiza kisasi kwa serikali ya Kenya baada ya kutuma vikosi vyake Somalia," alisema wakilituhuma kundi hilo kwa kujifanya wakimbizi kisha kuingia kambini hapo.

ALiongeza kuwa serikali imeongeza doria katika kambi na punde itafanya operesheni kuondoa wapiganaji hao.

Mwandishi wa BBC Bashkas Jugsodaay mjini Nairobi, anasema wakazi wa Dadaab walimwambia kuwa kuna ulinzi mkali wa majeshi ya usalma a katika kambi hiyo na polisi wameizingira hospital.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon alizuru Dadaab mapema mwezi huu, lakini hakuingia kambini humo kwa sababu za kiusalama.

Mlipuko wa karibuni umelenga polisi karibu na mpaka wa Somalia na Kenya.

Mapema mwezi huu polisi mmoja aliuawa na wengije watatu kujeruhiwa katika mlipuko kama huo karibu na Dadaab.