ICTR yahukumu wahusika wa Kimbari

Mahakama inayosikiliza kesi za uhalifu vitani imewahukumu vifungo vya maisha watu wawili walioandaa mauwaji ya kimbari nchini Rwanda mwaka 1994.

Image caption Hukumu kwa wakuu wa Rwanda

Hukumu hizo zimepitishwa dhidi ya watuhumiwa Matthieu Ngirumpatse na Edouard Karemera, waliokua wakuu wa kilichokua chama tawala cha nchini Rwanda.

Hukumu hio ilitolewa na Mahakama inayosimamiwa na Umoja wa Mataifa kuhusu mauwaji ya kimbari yaliyofanywa nchini Rwanda mnamo mwaka 1994.

Mnamo mwaka 1994 takriban watu 800,000 wengi wao kutoka kabila la Watutsi pamoja na Wahutu wenye misimamo ya wastani waliuawa katika kipindi cha siku 100.

Mahakama ya ICTR mjini Arusha iliamuru kua Ngirumpatse na Karemera walikua sehemu ya ushirikiano wa uhalifu wa pamoja ambao lengo lake lilikua kuwateketeza watu wa kabila ka Kitutsi.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Matthiew Ngirumpatse

Jaji aliyeongoza kesi hio Jaji Dennis Byron alisema kabla ya kumhukumu Ngirumpatse kwamba "mahakama hio ikakubaliana bila upinzani kumhukumu Ngirumpatse maisha jela."

'wasichana walibakwa' Ngirumpatse alikua Mwenyekiti wa kilichokua Chama tawala wakati huo cha National Revolutionary Movement for Development (NRMD) na Karemera alikua Naibu wake wakati wa mauwaji ya kimbari.

Hukumu hii ilibaini kua walikua na uwajibikaji wa juu kuamuru mauwaji ya kimbari, limearifu shirika la habari AFP.

Mahakama hio ya ICTR imeafiki kua Ngirumpatse alihakiki silaha ziwasilishwe katika hoteli moja ya mjini Kigali ambako kundi la Interahamwe lilikua mnamo mwezi April mwaka 1994.

"katika kipindi hicho wakati mauwaji yakifanyika, inafahamika kua silaha hizo bila shaka zilikua za kutuimiwa kwa mauwaji ya Watutsi, kwa mujibu wa maandishi ya Majaji katika Hukumu yao.

"mahakama hio imehitimisha kua visa vya ubakaji na uhalifu wote unaogusia jinsia dhidi ya wasichana wa Kitutsi na wanawake yakifanywa na askari na wanamgambo ikiwa ni pamoja na Interahamwe ni mchakato wa mambo ya kimaumbile ambayo yangebashiriwa katika mpango wa ushirika wa mauwaji ya kabila la Watutsi.