Rais Kabila kuiongoza DRCongo

Rais Joseph Klabila wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo aliapishwa jana kwa mhula wa pili kwenye sherehe iliyofanyika mjini Kinshasa.

Haki miliki ya picha
Image caption Kabila kuimarisha Umoja

Wakati akiapishwa Rais huyo aliahidi kulinda hadhi na Umoja wa kitaifa, huku mingurumo ya vifaru vya Kijeshi ikisikika katika maeneo mbalimbali ya mji kuzuia maandamano.

Bw.Kabila aliapishwa licha ya Mahakama ya juu ya nchi hio kusimamisha ushindi wake katika uchaguzi wa mwezi Novemba uliomalizika kwa ubishi.

Kiongozi wa upinzani Etienne Tshisekedi amesisitiza kua alishinda uchaguzi huo na kwamba yeye binafsi ataapishwa siku ya Ijumaa.

Uchaguzi huu ni wa kwanza kuandaliwa tangu mwisho wa vita vya wenyewe kwa wenyewe mnamo mwaka 2003, vilivyosababisha vifo vya takriban watu milioni nne.

Mwandishi wa BBC huko Congo, Thomas Hubert anasema Bw.Kabila mwenye umri wa miaka 40, alikula kiapo katika majengo ya Urais, kwenye sherehe ndogo iliyohudhuriwa na wafuasi wachache.

Mwandishi wetu anasema kua sherehe ya kumuapisha Bw.Kabila ilifanywa mbele ya majengo ya Mahakama kuu na alipokea mifano ya vitendea kazi vya kiasili kutoka kwa viongozi wa kijadi kama vile gozi yz chui na sanamu zilizochongwa.

Serikali iliitangaza siku ya jana kua ya mapumziko huku upinzani ukiwataka raia waandamane mjini Kinshasa na mingine ya Congo.

Ubelgiji ilisusiaRais Robert Mugabe wa Zimbabwe ndiye kiongozi pekee wa kigeni aliyehudhuria. Kwa mujibu wa mwandishi wetu- hio ni ishara ya kutoamini matokeo sababu kubwa iliyoanzishwa na mizengwe mingi iliyojitokeza wakati wa uchaguzi.

Wanabalozi walio nchini waliitwa kuhudhuria vinginevyo kuna uwezekano wakaombwa waondoke.

Bw. Kabila ameiongoza Congo tangu mwaka 2001 kufuatia kifo cha babake Laurent Desire Kabila.

Wiki iliyopita Bw Kabila alikiri kua kulikuepo na dosari katika mchakato wa uchaguzi, lakini akaongezea kusema kua matokeo yalithibitisha ukweli wa asili mia 100% na kupinga dhana ya kua matokeo yalikua na walakin.

Kituo chenye makao yake nchini Marekani cha 'Carter Center', kilichotuma waangalizi wake kwenye uchaguzi kilisema kua mizengwe iliyokuemo ilikua mingi kiasi kwamba hata matokeo hayaridhishi.

Wizara ya mashauri ya nje ya Marekani ilitaka uchunguzi ufanywe kuhusu mapungufu yaliyokuemo huku EU ikitaja sehemu ya mchakato mzima kama vurugu tupu.

Hata hivyo,Umoja wa Afrika ulitaja uchaguzi mzima kama mafanikio makubwa.