Viongozi wa Dunia kwenye mazishi

Viongozi wa Dunia wamekusanyika katika mji mkuu wa Jamhuri ya Czech kwa mazishi ya shujaa wa mapinduzi yaliyojulikana kama ''Velvet Revolution'' kutokana na jinsi mapinduzi hayo yalivyoendeshwa bila fujo Vaclav Havel.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mazishi ya Vaclav Havel

Kiongozi huyo alifariki jumapili akiwa na umri wa miaka 75.

Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy, Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron na Waziri wa mashauri ya nje Hillary Clinton na mume wakew, aliyekua Rais wa Marekani Bill Clinton, walijiunga na viongozi wengine kutoka nchi kadhaa ndani ya Kanisa la Mtakatifu Vitus.

Raia wote wapatao milioni 10.5 wa Jamhuri ya Czech walitazamiwa kusimama kwa dakika moja kama heshima kwa kiongozi wao huyo.

Katika nchi jirani ya Slovakia nako siku nzima ya Ijumaa ilitangazwa kua siku kuu na maombi yalifanywa mjini Prague yakiongozwa katika lugha mbili za Czech na Slovak.

Havel aliiongoza iliyokua Szechoslovakia kupitia mapinduzi ''hariri'' yaani Velvet ya mwaka 1989 yaliyouondoa utawala ulioungwa mkono na Soviet.

Mamiya ya raia wa Czech wamelipitia jeneza la Havel kanisani kutoa heshima zao. Wakuu walilazimika kuiacha milango waz hadi usiku wa manane kuwawezesha waombolwezaji wengi waweze kuliona jeneza la Havel.