Djibouti yatuma wanajeshi Somalia

Wanajeshi 100 wa Djibouti wamewasili Somalia kulipa nguvu jeshi la Umoja wa Afrika linalopambana na wapiganaji wa Kiislamu.

Haki miliki ya picha AP

Wanajeshi hao wamejumuika na wanajeshi wa Uganda na Burundi ambao tayari wako mji mkuu, Mogadishu.

Uchina imeupa Umoja wa Afrika zaidi ya dola milioni-nne kununua vifaa.

Wakati huo-huo wapiganaji wa Kiislamu wa al-Shabaab wamekuwa wakiajiri na kuwapa mafunzo wapiganaji zaidi, katika maeneo wanayodhibti nchini Somalia.