Kim aitwa kamanda mkuu kabisa

Kim Jong-un, kijana wa kiongozi wa Korea Kaskazini aliyefariki, Kim Jong-il, ametajwa kuwa kamanda mkubwa kabisa wa jeshi lenye nguvu la taifa hilo la kikoministi.

Haki miliki ya picha Reuters

Gazeti la chama tawala limetoa wito kwa Kim Jong-un aiongoze Korea Kaskazini kufikia ushindi wa daima.

Hii ni mara ya kwanza kwa shirika la habari la taifa kumtaja kiongozi huyo kuwa kamanda mkubwa kabisa.

Kabla ya hapo aliitwa mrithi mkubwa kabisa, baada ya baba yake kufariki.

Gazeti hilo limeahidi kuunga mkono sera iitwayo "songun", yaani jeshi ndio muhimu kabisa - sera inayoyapa kipa umbele matumizi juu ya jeshi la Korea Kaskazini.