Mbunge auwawa Afghanistan

Maafisa wa ngazi za juu Afghanistan wanasema kuwa watu kama 19 wameuwawa kwenye mripuko wa bomu katika mji wa Taloqan, kaskazini mwa nchi.

Haki miliki ya picha Reuters

Taloqan ni mji mkuu wa jimbo la Takhar.

Msemaji wa polisi wa huko alinukuliwa akisema kuwa bomu hilo liliripuliwa mazikoni, na aliyelengwa alikuwa mbunge, Mutalib Beg, ambaye alikufa katika mripuko huo.

Shambulio hilo lilifanywa na mtu aliyejitolea mhanga.