Wizara ya Iraq yashambuliwa

Mripuko mjini Baghdad juma lilopita Haki miliki ya picha AP

Watu kama saba wameuwawa katika shambulio la bomu dhidi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ya Iraq, mjini Baghdad.

Wakuu wanasema kuwa mabomu hayo yalirpiuliwa ndani ya gari na mtu aliyejitolea mhanga nje ya wizara.

Mripuko huo unafuatia miripuko mikubwa ya Alhamisi ambapo watu kama 70 walikufa.

Ghasia hizo zimezidisha mvutano wa kisiasa na kidini ambao umetokeza tena baada majeshi ya Marekani kuondoka mwezi huu.

Makamo wa rais wa Marekani, Joe Biden amewaelezea viongozi wa Iraq, kwamba anatiwa wasi-wasi na ghasia hizo.