Rais Saleh ataka kwenda Marekani

Serikali ya Rais Obama inasema kuwa inazingatia ombi la Rais Ali Abdullah Saleh wa Yemen, kutaka kwenda Marekani.

Haki miliki ya picha Reuters

Ijumaamosi, Bwana Saleh alisema ataondoka nchini kwenda Marekani, ili kuzimua ghasia nchini mwake.

Alisema safari hiyo, siyo ya kupata matibabu kwa majaraha aliyopata katika jaribio la kumuuwa mwezi wa Juni.

Lakini afisa wa Marekani alisema ombi la Bwana Saleh linazingatiwa kwa sababu za kimatibabu.

Ghasia zimeendelea nchini Yemen, ingawa Rais Saleh alikubali kuondoka madarakani mwezi uliopita.