Waandishi wa habari wafungwa Ethiopia

Waandishi wa habari wa Sweden waliokamatwa Ethiopia Haki miliki ya picha AFP

Mahakama nchini Ethiopia, yamewahukumu waandishi wa habari wawili kutoka Sweden, kifungo cha miaka 11 kwa kukisaidia kikundi kilichopigwa marufuku cha wapiganaji wa Ogaden, ONLF; na kwa kuingia nchini bila ya kibali.

Mwandishi wa habari, Martin Schibbye na mpiga picha Johan Persson walikamatwa mwezi wa July, baada ya kuingia eneo la Ogaden la Ethiopia.

Wakili wa washtakiwa hao anasema hukumu hiyo ni ya kikatili kwa watu wasiokuwa na hatia.