Washukiwa ugaidi waachiliwa Kenya

Polisi wa Kenya wakilinda maduka Nairobi Haki miliki ya picha Reuters

Polisi nchini Kenya wamewaachilia huru bila mashtaka washukiwa wawili ambao walikamatwa na kikosi cha kupambana na ugaidi nchini humo.

Watu hao ambao ni raia wa Kenya na picha zao zilisambazwa kwa umma kabla, walijisalimisha wenyewe kwa wakuu Jumamosi iliopita.

Vita dhidi ya ugaidi nchini Kenya vimekosolewa, huku polisi wakishutumiwa kutokuwa makini katika uchunguzi wao .

Msemaji wa polisi nchini Kenya, Eric Kiraithe aliiambia BBC, kwamba bado wako imara katika kupambana na ugaidi licha ya washukiwa hao kuachiliwa huru.