Wachunguzi waanza kazi Syria

Luteni Jenerali Mohammad al_dabi wa Sudan anaongoza ujumbe wa Kiarabu Syria Haki miliki ya picha Getty

Ujumbe wa Jumuia ya nchi za Kiarabu unaanza kazi yake nchini Syria kuchunguza makubaliano mepya ya kumaliza ghasia nchini humo.

Wanaharakati wanasema baadhi ya vifaru vya serikali ya Syria vimeanza kuondoshwa katika mji wa Homs, ambako kwa miezi kadha kumekuwa na mapambano na waandamanaji wanaopinga serikali, na watu kadha wameuwawa.

Ujumbe huo unasema utakwenda kujionea hali ilivyo huko Homs.

Inaarifiwa kuwa watu kama 30 waliuwawa Jumatatu katika ghasia za karibuni kabisa.

Umoja wa Mataifa unasema watu zaidi ya 5000 wameuwawa tangu maandamano dhidi ya serikali kuanza nchini Syria mwezi wa March.